Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Marekani yachangia misaada ya mlo wa shuleni Cote d’Ivoire

Marekani yachangia misaada ya mlo wa shuleni Cote d’Ivoire

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula WFP limekaribisha mchango wa dola milioni 35.6 uliotolewa na Marekani kwa ajili ya miradi ya mlo wa shuleni nchini Cote d’Ivoire.

Taarifa ya WFP imesema kwamba mchango huo utawezesha WFP kuwapatia kila siku watoto 125,000 wa shule 600 za msingi za serikali chakula cha moto kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Mradi huo unalenga maeneo yaliyo kwenye mazingira magumu zaidi, ukiwezesha pia wakulima wanawake kushirki huo mradi na kuziuzia shule husika vyakula wanavyohitaji.

WFP imeeleza kwamba miradi ya mlo wa shuleni kusaidia kupunguza utapiamlo na kuvutia watoto kusoma.