Skip to main content

Njaa na utapiamlo vyazidi kushika kasi Somalia- OCHA

Njaa na utapiamlo vyazidi kushika kasi Somalia- OCHA

Hali ya ukosefu wa uhakika wa chakula na utapiamlo inazidi kutishia Somalia wakati huu ambapo watu wapatao Milioni Tatu nukta Saba wanatarajiwa kukumbwa na hali hiyo hadi katikati ya mwaka huu.

Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu nchini Somalia Peter de Clercq amesema kiwango cha utapiamlo miongoni mwa watoto kinatia hofu ambao zaidi ya watoto Laki Tatu wanakabiliwa na unyafuzi.

Amesema hofu inazingatia kuwa watoto Elfu 58 kati ya hao wako hatarini kufariki dunia iwapo hawatapatiwa tiba na lishe sahihi.

Bwana de Clercq amesema huku ukame ukizidi kushika kasi kwenye maeneo ya Puntland na Somaliland, watu wengi zaidi wako hatarini kutumbukia kwenye baa la njaa na utapiamlo.