Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

David Dube msanii wa hiphop wa DRC aimba kuhusu ukatili wa kingono : MONUSCO

David Dube msanii wa hiphop wa DRC aimba kuhusu ukatili wa kingono : MONUSCO

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO umezindua kampeni ili kuelimisha jamii kuhusu ukatili wa kingono na hasa kupinga ukwepaji sheria ambao umeenea nchini humo.

Wakati ambapo machafuko yameongezeka mashariki ya kati na hivyo ripoti za mateso ya raia, ujumbe kupitia wimbo wa David Dube na video yake umesambazwa na kushawishi watu kuvunja ukimya kuhusu uhalifu huo.

Ungana na Priscilla Lecomte kwenye makala hii.