Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kenya imepiga hatua katika vita dhidi ya ukeketaji:UNFPA

Kenya imepiga hatua katika vita dhidi ya ukeketaji:UNFPA

Tarehe sita Februari kila mwaka ni siku ya kimataifa ya kupinga ukeketaji na mwaka huu kauli mbiu ni ‘tutokomeze ukeketaji sasa”. Taarifa kamili na Flora Nducha.

(Sauti  ya Flora)

Nchi mbalimbali zimekuwa zikichukua hatua ikiwa ni pamoja na kuelimisha umma, na wadau wote wakiwemo mangariba. Kampeni kubwa inafanywa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu( UNFPA) kwa kushirikiana na nchi husika.

Florence Gachanja ni Afisa Mipango wa UNFPA Kenya anasema mbali ya elimu,  sheria pia imechangia kwa Kenya.

(SAUTI YA FLORENCE)

Kenya imepunguza ukeketaji kutoka asilimia 82 Mwaka 2003 hadi asilimia 21 mwaka 2014.