Jumuiya ya Kimataifa ilaumiwe kwa mzozo wa Syria:Ban
Mkutano kuhusu uhisani kwa ajili ya Syria ukiwa umeanza leo mjini London, Uingereza, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema jumuiya ya kimataifa inapaswa inalaumiwa na inawajibika kwa kushindwa kutanzua mzozo wa Syria uliongia mwaka wa sita.Taarifa kamili na Grace Kaneiya.
(Taarifa ya Grace)
Akiongea wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, Ban amesema mkwamo wa mazungumzo ya kusaka amani yaliyositishwa juma hili mjini Geneva unaonyesha mgawanyiko mkubwa kwa waSyria na akaongeza.
(SAUTI BAN)
‘‘Inasikitisha sana kwamba hatua za awali za mazungumzo zimekwamishwa na kuendelea kuzuiliwa ufikishwaji wa misaada ya kibinadamu, na kuongezeka ghafla kwa mabomu ya angani na shughuli za kijeshi ndani ya Syria.’’
Katika hatua nyingine Katibu Mkuu ametaja mambo matatu ambayo ni malengo ya mkutano huo kuwa ni kufikia mahitaji ya kibinadamu ambayo ni dola bilioni saba kwa mwaka huu pekee, ikiwa ni mara mbili ikillinganishwa na mwaka jana,kuweka msingi wa usaidizi wa kimataifa na kutafuta namna ya kusaidia raia.