Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana wasiwe wanufaika tu, waamue wenyewe miradi yao: kongamano la vijana

Vijana wasiwe wanufaika tu, waamue wenyewe miradi yao: kongamano la vijana

Leo kongamano la vijana likifikia ukingoni jijini New York, Marekani, azimio linatarajiwa kupitishwa ambalo litajumuisha mapendekezo ya vijana zaidi ya mia nane waliohudhuria mkutano huo uhusu jinsi ya kushirikishwa kwenye utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu SDGs.

Akihojiwa na idhaa hii, Laurence Muli, mtalaam wa maswala ya kisiasa na mazingira kutoka Kenya anayefanya kazi na sekretarieti ya jumuiya ya Commonwealth nchini Uingereza amesema vijana wamependekeza washirikishwe zaidi kwenye uongozi:

(Sauti ya Lawrence)

Aidha amesisitiza umuhimu wa serikali za Afrika Mashariki kuwapatia vijana fursa za ajira na hasa za kuanzisha biashara yao wenyewe kupitia mikopo.

(Sauti ya Lawrence)