Dola Milioni 100 za CERF kusaidia wakimbizi na wenye dharura, Tanzania mojawapo

29 Januari 2016

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akiwa Ethiopi, leo ametangaza kutoa dola Milioni 100 kutoka mfuko wa kushughulikia majanga, CERF kwa ajili ya operesheni za usaidizi wa kibinadamu zinazokabiliwa na ukata ikiwemo Afrika.

Maeneo ya Afrika ni pamoja na Mashariki na Kati mwa bara hilo ambapo Ban amesema fedha zitasaidia mamilioni ya wahitaji waliolazimika kung’oka makwao kutokana na mizozo ikiwemo warundi 126,000 waliolazimika kuondoka kwao na kuelekea Tanzania tangu mwezi Aprili mwaka jana.

Tanzania ni moja ya wanufaika ambapo mwakilishi mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini humo Alvaro Rodriguez amezungumza na Idhaa hii na kutaja kiwango itakachopokea na matumizi..

(Sauti ya Alvaro)

Mahitaji ya kibinadamu ni pamoja na mipango ya kuepusha ukatili wa kingono na upatikanaji wa chakula na huduma za afya.

Kwa mujibu wa Alvaro kila wiki wanapokea wakimbizi 1500 kutoka Burundi na kwamba suluhu la kudumu la kisiasa ndio muarobaini ili wakimbizi waweze kurejea makwao.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud