Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake Afrika waneemeka na ADB

Afisa mawasiliano wa Benki ya Maendelo  ya Afrika akihojiwa na Idhaa ya Umoja wa Mataifa New York City

Wanawake Afrika waneemeka na ADB

Shirika la Umoja wa mataifa linalohusika na masuala ya wanawake UN Women kwa ushirikiano na Bank ya maendeleo Afrika ADB wameanzisha mpango wenye lengo la kuwakwamua wanawake barani Afrika kutoka kwenye umasikini

Hayo yamesemwa na Cynthia Kamikazi afisa mawasiliano wa ADB alipohojiwa na Idhaa ya kiswahili ya Umoja wa Mataifa alipozuru kwenye makao makuu jijini New York.

Bi Cinthya amesema benki ya ADB imetenga fungu maalumu la fedha zitakazotumikakutoa mikopo yenye riba nafuu kwa wanawake ili kuwawezesha kujikwamua katika umasikini barani Afrika.

(Sauti ya Cynthia Kamikazi-CUT 1)

“Mpango huu umeratibiwa ili kuwazesha kiuchumi haswa wanawake, na kupitia mpango huu pia tuna mikakati ya kuwawezesha wanawake walio katika uongozi kama bungeni na kdhalika ili waweze kupitisha sheria za usawa kwa wanawake. Tumeona juhudi za UN Women katika kusimamia haki sawa kwa wanawake katika bara la Afrika. Na hii ni sababu kubwa tumekuja hapa makao makuu.

Akifafanua kuhusu mikakati hiyo bi Cinthya amesema…..

(Sauti ya Cynthia-CUT 2)

Bank imetoa kiasi cha dola milioni 300 zitakazo tumika katika mikopo kwa wanawake kwa lengo la kuzalisha bilioni 3 kwa muda wa miaka 10 . Na sehemu ya pili ni uwekezaji katika miradi itakayosaidia maendeleo ya wanawake barani Afrika ili kuhakikisha wanawake wanadhaminiwa. Ili kufanikisha hilo tunafanya kazi na wanawake viongozi walioko bungeni kupitisha sheria zitakazowapatia wanawake haki ya umiliki wa ardi au mali zitazowapa dhamana wakati wanahitaji mikopo.