Mbinu za kisasa zahatarisha kutoweka kwa aina asilia za wanyama:FAO

27 Januari 2016

Ripoti mpya ya shirika la chakula na kilimo duniani, FAO imesema kitendo cha wafugaji na watunga sera duniani kote kuvutiwa na mbinu za kisasa ili kuwa na aina bora ya wanyama katika zama za sasa za ongezeko la joto duniani kunatishia uwepo wa mbegu asilia za wanyama.

FAO imesema jamii zinatumia mbinu kama vile kuchanganya mbegu za wanyama ili kupata mbegu bora na kuhakikisha upatikanaji wa chakula lakini kuna matukio ambapo wataalamu na wafugaji wanapendezewa na aina moja zaidi.

Beate Scherf ni afisa wa masuala ya wanyama FAO anasema kuna aina 38 tofauti za wanyama kama vile ng’ombe, kondoo, sungura, na kadhalika lakini kuna hatari hasa katika nchi zinazoendelea ambako kumeripotiwa changamoto katika kutumia mbegu za kisasa za wanyama na kuku kutokana na uingizwaji holela wa mbegu hizo..

(Sauti ya Beate)

“Mbegu hizi za kisasa za wanyama  zinapunguza uwezo wa wanyama asili waliozoea mazingira. Ni kweli mbegu za kisasa zinazalisha mayai mengi, maziwa na hata nyama bora na zinaonekana na faida zaidi, lakini kwa upande mwingine  zinahitaji matunzo  zaidi ikiwemo chakula na mara nyingine wanyama au kuku wanaweza wasitoe mazao, na hata hukumbwa na magonjwa mara kwa mara na hata kufa, kwa hiyo ni hasara zaidi kwa mfugaji.”

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter