Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa sanyansi na teknolojia wa UNISDR umeanza leo Geneva

Mkutano wa sanyansi na teknolojia wa UNISDR umeanza leo Geneva

Mkutano wa sayansi na teknolojia wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya upunguzaji wa hatari ya majanga UNISDR umeanza leo mjini Geneva kwa kuwaenzi mamia ya wanasayansi ambao wamechangia muda wao kwa utafiti kuhusu mabadiliko ya tabianchi na athari zake.

Mkuu wa UNISDR bw. Robert Glasser, amesema kazi ya mamia ya wanasayansi waliochangia kwenye jopo la kimataifa la mabadiliko ya tabia nchi ni mfano bora dhahiri wa huduma kwa umma na kujitolea kwa mambo mema yanayotarajiwa kutoka kwa jumuiya ya kimataifa ya wanasayansi.

Mkutano huo wa siku tatu una lengo la kuimarisha ushirikiano Zaidi kwa ajili ya utekelezaji wa mkataba wa Sendai na kusaidia katika uelewa wa upunguzaji wa hatari ya majanga katika makubaliano mingine ya kimataifa. Katika siku ya kwanza leo watu 700 wameshiriki wakiwemo wanasayansi, wataalamu wa kupunguza hatari za majanga na wawakilishi wa serikali.

Bw,. Glasser amesema hadio wmisho wa wiki kutakuwa na matokeo mawili muhimu, ambayo ni uzinduzi wa njia ya ushirika na muafaka wa sayansi na teknolojia wa UNISDR kwa ajili ya utekelezaji  wa mkataba wa Sendai mkutano huo unaungwa mkono na wadau na mashirika mengine ya Umoja wa mataifa yakiwemo UNESCO, WMO,Chuo Kikuu cha Umoja wa mataifa na WHO.