Nishati bunifu ni suluhu ya athari za mabadiliko ya tabianchi- Dkt. Han

Nishati bunifu ni suluhu ya athari za mabadiliko ya tabianchi- Dkt. Han

Huko Abu Dhabi, Falme za kiarabu, wataalamu wamekuwa na mjadala kuhusu jinsi ubunifu kwenye nishati unaweza kusaidia kuhimili athari za mabadiliko ya tabianchi wakati huu ambapo tayari nchi wanachama wa UM zimepitisha mkataba mpya wa kudhibiti mabadiliko hayo.

Akizungumza kwenye mjadala huo Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika kupunguza athari za majanga, Dkt. Han Seun-Soo amesema hakuna shaka kuwa dunia sasa inashuhudia athari za mabadiliko hayo ikiwemo vimbunga, mafuriko na hali ya hewa ya kupitiliza kwa hiyo..

(Sauti ya Dkt. Han clip)

"Kwahiyo tunachojaribu kufanya hapa ni kushughulikia tatizo hili kupitia uvumbuzi wa nishati, na kama unavyofahamau Abu Dhabi iko mstari wa mbele katika kusukuma maendeleo ya nishati mbadala kwa miaka kadhaa iliyopita na hili limefanaikiwa hadi sasa."