Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zaidi ya dola milioni 800 zahitajika Somalia- OCHA

Zaidi ya dola milioni 800 zahitajika Somalia- OCHA

Jumuiya ya masuala ya kibinadamu nchini Somalia leo imezindua mpango wa masuala ya kibinadamu ya kuyapa kipaumbele mwaka 2016 (HRP) mjini Mogadishu, ukitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuhakikisha ufadhili unaohitajika na kwa wakati. Amian Hassan na taarifa kamili.

(Taarifa ya Amina)

Mpango huo mpya unatafuta dola milioni 885 ili kuwafikia watu milioni 3.5 wanaohitaji msaada wa haraka wa kuokoa maisha kufikia mwishoni mwa mwaka 2016.

Kenneth Odiwuor ni Afisa wa Habari na Mawasiliano OCHA Nairobi na hapa anaelezea umuhimu wa msaada huo..

(Sauti ya Kenneth)

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya dharura na masuala ya kibinadamu OCHA, mpango huo unakuja wakati kuna mahitaji makubwa ikikadiriwa kuwa watu zaidi ya milioni 4 wanahitaji msaada wa kuokoa maisha huku wakimbizi wa ndani zaidi ya milioni moja wamesubiri saana kupata suluhu ya jinamizi linalowakabili.