Skip to main content

Misaada yapaswa kuwafikia walengwa Syria hima:UM

Misaada yapaswa kuwafikia walengwa Syria hima:UM

Umoja wa Mataifa umetaka umetoa wito wa kuondolewa vikwazo vya kufikisha misaada kwa takribani watu laki nne wanaozingirwa na makundi kinzani ya machafuko nchini Syria.

Kwa mujibu wa mwakilishi mkazi wa ofisi ya UM ya kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA nchini humo Yacoub El Hillo, wito huo unafuatia mwitikio kidogo wa makundi kinzani ambapo mwaka jana ni asilimia 10 tu ya maombi ya misafara ya misaada yaliruhusiwa kuwafikia wahitaji huku maelfu zaidi bado wakikabiliwa na njaa.

Taarifa kutoka maeneo hayo zinasema kwamba watu wanakufa kutokana na njaa na wengine wakiuwawa wakati wakijaribu kutoroka mathalani Januari tano mzee wa miaka 53 alifariki kutokana na njaa huku familia yake ya watu watano ikiendelea kuteseka na utapiamlo.

(SAUTI YACOUB)

Zaidi ya watu milioni nne wanaishi katika maeneo ambayo hayafikiki kutokana na machafuko yanayoendelea nchini Syria