Suluhu kwa migogoro kupunguza kadhia ya wahamiaji duniani: Grandi

4 Januari 2016

Kamishna Mkuu mpya wa shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi UNHCR Filippo Grandi, amesema ana matumaini ya kupatikana suluhisho la migogoro kwa kushughulikia mizizi ya vyanzo vyake ili kupunguza wimbi kubwa la wakimbizi na wahamiaji linaloikabili dunia . Taarifa kamili na Grace Kaneiya

(TAARIFA YA GRACE)

Akiongea mjini Geneva Uswisi katika siku yake ya kwanza kukaimu madaraka kutoka kwa aliyekuwa Kamishna Mkuu António Guterres,  Bwana Grandi amesema UNHCR inakabiliana na changamoto kadhaa kufuati migogoro inayosababisha kadhia ya wahamiaji huku kukiwa na pengo kubwa kati ya mahitaji ya kibinadamu na rasilimali.

Amesema changamoto nyingine aliyoiita hatari ni chuki dhidi ya wageni lakini akasema kuwa anatarajia ushirikiano baina ya shirika analiloingoza na serikali, asasi za kiraia na wadau wengine utapiga hatua za kuhakikisha ulinzi wa kimataifa na kuimarisha mazingira ya maisha kwa mamilioni ya wakimbizi.

Kamishina Grandi mwenye uzoefu katika mausala ya misaada ya kibinadamu amesisitiza kuwa UNHCR itashirikiana na kila ambaye lengo lake ni kusaka suluhu ikiwa ni sehemu ya wajibu mkuu wa shirika hilo.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter