Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wasaka hifadhi kutinga nchi zilizoendelea kulizua mjadala: Guterres

Wasaka hifadhi kutinga nchi zilizoendelea kulizua mjadala: Guterres

Kamishna Mkuu wa Shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR, aliyemaliza muda wake António Guterres, ambaye amehudumu katika nafasi hiyo kwa miaka 10 amezungumzia changamoto zinazokabili shirika hilo wakati huu ambapo wahamiaji na wakimbizi ni changamoto ya dunia.

Bwana Guterres ambaye pia amezungumzia  uzoefu wake katika kipindi cha uongozi akisema dunia imeshuhudia viwango vya juu vya ufurushwaji wa watu katika miaka ya hivi karibuni kuanzia 2010 hadi 2015. Idadi ya watu wanaokimbia makwao kufuatia ghasia imeongezeka mara nne, kwa sababu ya mizozo mipya na mizozo ya awali na hamna suluhu.

Ameongeza kwamba kumekuwa na ongezeko la watu wanokimbia na ghadabu itokanayo na hali hiyo. Hayo yote yamefanyika bila kuibua hisia au mazungumzo katika ngazi za kimataifa lakini hali ilibadilika.

(SAUTI GUTERRES)

“Kwa mara moja, suala la wakimbizi lilpewa kipaumbele katika mazungumzo ya jamii ya kimataifa cha kusikitisha ni kwamba sababu ya mazungumzo hayo ilikuwa ni kwa sababu wakimbizi walikimbilia mataifa yaliyostawi, hii ina maana kwamba watu walikuwa wanasikitikia zaidi mataifa hayo na wala sio wakimbizi, lakini hii pia inatoa fursa .’’