Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya wakimbizi wa ndani yaongezeka mwaka 2015 : UNHCR

Idadi ya wakimbizi wa ndani yaongezeka mwaka 2015 : UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa ka Kuhudumia Wakimbizi UNHCR limeonya leo kwenye taarifa yake kwamba mwaka 2015 huenda utavunja rekodi kuhusu idadi ya watu waliolazimika kuhama makwao duniani kote. Ripoti ya nusu ya mwaka ya UNHCR iliyotolewa leo inaonyesha kwamba idadi ya waliolazimika kuhama makwao itazidi milioni 60 mwaka huu, kwa mara ya kwanza katika historia.Sababu ya ongezeko hilo kwa mujibu wa UNHCR ni mizozo inayoikumba Syria na maeneo mengine duniani, takwimu zikionyehsa kwamba takriban watu 4,600 wamekimbia nchi zao kila siku kwa kipindi cha miezi sita ya kwanza ya mwaka 2015.

Matokeo ya ongezeko hilo ni shinikizo la kiuchumi na kibinadamu kwa nchi zinazopokea makimbizi, nyingi zikiwa ni nchi zinazoendelea. Aidha wimbi la wakimbizi limesababisha pia mivutano ya kisiasa kwenye nchi zilizopokea wakimbizi wengi.