Jumuiya ya kimataifa ichukue hatua kuepusha vita vya wenyewe kwa wenyewe Burundi: Zeid

17 Disemba 2015

Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa mataifa Zeid Ra’ad Al Hussein leo ameitaka jumuiya ya kimataifa kuchukua maamuzi na hatua imara kuhusu hali ya Burundi ili kuepusha vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vinaweza kuwa na athari kubwa katika kanda nzima. Assumpta Massoi na taarifa zaidi.

(Taarifa ya Assumpta)

Akizungumza kwenye majadala maalumu kuhusu Burundi kwenye baraza la haki za binadamu amesema Burundi imefika pabaya

(SAUTI YA ZEID)

Burundi iko katika hatua ya mpasuko, manusra ya vita vya wenyewe kwa wenyewe .Mauaji ya wiki iliyopita yanathibitisha kiwango ambacho ghasia na vitisho vinairudisha nchi hiyo nyuma , miaka ambayo ilighubikwa na  Burundi huzuni, giza na vurugu za kutisha sana"

Amesema wakati wa hatua za polepole na kujizungushazungusha umekwisha sasa ni wajibu wa jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua. Takribani watu 400 wameuawa tangu April 26, wengine 3496 wakiswekwa rumande na wengine 220,000 sasa ni wakimbizi katika nchi jirani na maelfu kuwa wakimbizi wa ndani.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter