Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Naungana na Ban katika nia ya kukomesha unyonyaji na unyanyasaji wa kingono:Zeid

Kamishina Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Maifa Zeid Ra’ad Al Hussein akitoa kauli leo kufuatia ripoti huru yaunyanyasaji wa kingondo dhidi ya vikosi vya kulinda Amani vya kimataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, amesema anamuunga mkono Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika nia ya kutokomeza unyonyaji na unyanyasaji wa kingono kwa vikosi vyote vya kimataifa vya kulinda Amani, vya Umoja wa mataifa na visivyo vya Umoja wa mataifa. Na pia kutatua udhaifu uliobainika na jopo huru.

Amesisitiza juu ya haja ya wakati wote kuweka ulinzi wa wahanga hususani watoto msitari wa mbele. Amesema anaamini bado kuna kazi ya kufanya hasa nan chi wanachama ili kuuwezesha Umoja wa Mataifa kukomesha vitendo hivyo vya unyonyaji na unyanyasaji wa kingono unaofanywa na baadhi ya vikosi vya Umoja wa mataifa na wafanyakazi wa kiraia, pamoja na vikosi visivyo vya Umoja wa Mataifa .

Amesema lazima uchunguzi dhidi ya unyanyasi wa kingono ufanywe kwa utaratibu na ufanisi na wale waliohusika waadhibiwe. Amesema anaamini pia ni muhimu kwa mfumo wa Umoja wa mataifa kwa ujumla uimarike na kuchochea kasi ya kuchukua hatua dhidi ya aina zote za ukiukaji wa haki za binadamu.