Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Inteneti na mitandao ya kijamii inasaidia ISIL kusajili wapiganaji 30,000

Inteneti na mitandao ya kijamii inasaidia ISIL kusajili wapiganaji 30,000

Kundi la kigaidi la ISIL limetumia interneti na mitandao ya kijamii kusajili wapiganaji angalau 30,000 wa kigeni kutoka nchi Zaidi ya 100 kwende kupigana Syria na Iraq.

Hii ni kwa mujibu wa maafisa wa Umoja wa mataifa waliozungumza kwenye mkutano maalumu unaododosa matumizi ya teknolojia yanayofanywa na makundi ya kigaidi.

Jean-Paul Laborde ni mkurugenzi mkuu katika kurugenzi ya kupambana na ugaidi anasema ni kwa nini mkutano huu ni muhimu.

(SAUTI LABORDE 1)

"Ni muhimu sana kwa sababu ni mkutano wa kwanza ambapo tunao wote pamoja: sekta binafsi , nchi wanachama na asasi za kijamii. Tunahitaji pande zote tatu hatuwezi kufanya kazi na mojawapo tu , sekta binafsi au nchi wanachana au asasi za kijamii."

Pia amefafanua matarajio yao

(SAUTI LABORDE2)

"Natarajia hatua miongoni mwa pande hizi tatu kuwa na mpango maalumu kwa dhamira ya kuimarisha uwezo wa kukabiliana na uchagizaji wa ugaidi na usajili wa wapiganaji wa kigeni."