Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IFAD kutoa fursa ya chakula kwa maelfu Afghanistan

IFAD kutoa fursa ya chakula kwa maelfu Afghanistan

Mfuko wa kimataifa kwa ajili ya maendeleo ya kilimo IFAD umetia saini mkataba na serikali ya Afghanistan ambao utasaidia kuhakikisha usalama wa chakula na kuinua hali ya uchumi kwa maelfu ya wakazi wa vijijini katika taifa hilo linalokabiliwa na upungufu wa chakula kila mara.

Msaada huo unaojumuisha dola milioni 48.5 kutoka IFAD  una lengo la kuboresha maisha na kuwapa kaya 57,000 katika wilaya sita kwenye majimbo ya Balkh, Herat na Nangarhar .

Kwa mujibu wa rais wa IFAD Kanayo F.Nwanze fedha zingine milioni 2.5 zitatolewa na

kitengo cha ufadhili wa fedha cha Afghanistan huku serikali ikifadhili dola milioni 3.8.

Ushirika huo mpya utajikita katika uwezo wa taasisi za Afghanistan ili kutoa huduma za maendeleo ya kilimo , pamoja na kuimarisha uzalishaji, niundombinu na masoko ili kuongeza kipato cha wakulima wadogowadogo.