Skip to main content

Wakati jumuiya ya LGBT inateseka "sisi wote tunaathirika:OHCHR

Wakati jumuiya ya LGBT inateseka "sisi wote tunaathirika:OHCHR

Wakati jumuiya ya watu wa mapenzi ya jinsia moja, mashoga, wasagaji na waliobadili jinsia (LGBT) wakinyimwa haki zao katika jamii jamii sote katika jamii tunaathirika. Hayo ni kwa mujibu wa Charles Radcliffe,wa ofisi ya kamishina mkuu wa haki za binadamu.

Radcliffe ameyasema hayo Alhamisi katika maadhimisho ya siku ya haki za binadamu akitanabaisha gharama za kiifedha na kijamii zitokanazo na kuibagua jumuiya ya LGBTduniani kote.

Na katika maadhimisho hayo Umoja wa mataifa umetoa mkanda wa video uitwao “gharama za kutengwa” uliokaririwa na muigizaji maarufu wa star Trek Zachary Quinto. Bwana Radcliffe amezungumza na Radio ya Umoja wa mataifa kuhusu ujumbe wa video hiyo

(SAUTI YA RADCLIFFE)

“Hatua ya kwanza ni kuhamasisha na kuwafanya watu waanze kuzungumzia masuala haya, na unapaswa kufanya hivyo kwa njia tofauti. Huwa tunazungumza kuhusu ukatili na ubaguzi kama ukiukaji wa haki za binadamu, na kila nchi mwanachama wa Umoja wa Mataifa, ina wajibu wa kisheria wa kulinda haki za binadamu. Lakini huu ni wigo mwingine, na tunasema, tizama, una wajibu huu wa kisheria, na juu ya hayo, katika kutoutimiza, inakugharibu kiuchumi na kuigharimu jamii yako. Nadhani taarifa na mjadala huu utasaidia kubadilisha hali, na natumai kuwa tutaongeza kasi ya mabadiliko katika nchi ambazo bado zina ukinzani.”