Skip to main content

COP21 ikikaribia ukingoni, jamii asilia zapasa sauti

COP21 ikikaribia ukingoni, jamii asilia zapasa sauti

Ikiwa zimesalia siku mbili kabla ya kukamilika mwa mkutano wa mabadiliko ya tabianchi huko Paris, UFaransa, imeelezwa kuwa rasimu ya awali ya mkataba inatarajiwa baadaye leo, na iwapo itaridhiwa, itakamilishwa tayari kwa kutiwa saini Ijumaa.

Wakati hayo yakiendelea, washiriki kutoka jamii ya watu wa asili wamesema hawaridhishwi na mchakato wa majadiliano, wakidai umeweka kando  jamii zao hususani ni wafugaji na wakusanya matunda.

Katika  mahojiano na redio ya Umoja wa Mataifa mjini Paris, Gideon Sanago ambaye ni mwakilishi wa jamii ya wafugaji wamasai kutoka Simanjiro Tanzania, amesema wameamua kukutana na Rais wa COP 21 ili kueleza kilio chao kwa kuwa.

(SAUTI GIDEON)

Amesema kwa kiaasi kikubwa jamii zao zimeathiriwa na mabadiliko ya tabianchi akitolea mfano wa mifarakano kati ya wafugaji na wakulima kutokana  na kuhamahama kusaka malisho ya mifugo baada ya mabadiliko ya tabianchi.