Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kampeni ya kupambana na ukatili dhidi ya watoto yazinduliwa Afrika Mashariki

Kampeni ya kupambana na ukatili dhidi ya watoto yazinduliwa Afrika Mashariki

Mashirika ya Kimataifa yamezindua leo kampeni ya kupambana na ukatili dhidi ya watoto kwenye ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini. Taarifa zaidi na Joseph Msami.

(Taarifa ya Msami)

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF ni moja ya mashirika hayo, ambapo kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo, wasichana wawili kati ya watano wenye umri wa chini ya miaka 18 kwenye ukanda huo wameathirika na ukatili wa kingono, huko asilimia 70 ya watoto wakiripoti kupigwa nyumbani au shuleni.

Taarifa imesema ukatili huo unaweza kuathiri mtoto kwa maisha yake yote na kuzuia maendeleo yake kiakili na kimwili.

Kampeni inalenga kubadilisha tabia za jamii na kushawishi serikali kuwekeza katika sera na huduma kwa ajili ya watoto, kama vile kamati za ulinzi wa watoto, namba za simu za kupiga muda wowote au vituo vya polisi rafiki kwa watoto.