Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kiwango cha elimu na uhusiano katika tija: Ripoti

Kiwango cha elimu na uhusiano katika tija: Ripoti

Ripoti mpya ya shirika la kazi duniani, ILO imeonyesha kuwa kiwango cha elimu ya wafanyakazi kinaimarika lakini kupata elimu ya juu siyo tiketi ya kupunguza ukosefu wa ajira duniani hususan nchi za kipato cha kati na chini.

Ikipatiwa jina viashiria muhimu katika soko la ajira, ripoti hiyo imetolea mfano nchi za kipato cha kati na cha chini ambako kuwa na elimu ya juu hakumaanishi kuwa mtu atapata ajira.

Hata hivyo Steven Kapsos  ambaye ni Mkuu wa kitengo cha uchambuzi takwimu, ILO anasema nchi 62 kati ya 64 zilizoangaziwa takwimu zinazoonyesha wenye elimu ya juu wanapata ajira hususan Urusi, Canada na Luxembourg na hiyo ni habari njema kwa kuwa ….

(Sauti ya Steven)

Kwanza kwa wafanyakazi wenyewe kwani wale waliosoma zaidi wananufaika na mapato ya juu na mazingira bora ya kazi na hivyo kuunga mkono manufaa ya moja kwa moja kwa wafanyakazi katika nchi  hizo. Na pili takwimu zinaonyesha uhusiano thabiti kati ya kiwango cha elimu walichonacho wafanyakazi na kiwango cha tija kitaifa.”