Skip to main content

UNESCO yaja na mfumo mpya wa hamasa na mabadiliko

UNESCO yaja na mfumo mpya wa hamasa na mabadiliko

Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni UNESCO limezindua mbinu mpya ya kueleza hadithi za kuleta mabadiliko na hamasa wakati wa mkutano mkuu wa shirika hilo sambamba na maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.

Kupitia video inayoonyesha hatua mbalimbali zilizopigwa katika majukumu ya msingi ya UNESCO, shirika hilo linaonyesha njia bunifu za lugha muono ambayo huleta majadiliano na ufahamu kwa ajili ya kupigia chepuo amani na mabadiliko.

Ubunifu huo ambao ni sehemu ya maonesho yaliyowezeshwa na wadau kadhaa wakiwamo taasisi iitwayo Li Ka Shing Foundation na UNESCO imetoa fursa kwa wasomaji na watazamaji kuona matukio na maonyesho kupitia tovuti hii www.mosaicofchange.org.