Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uwazi na uwajibikaji watangazwa kanuni mpya ya Rais wa Baraza Kuu

Uwazi na uwajibikaji watangazwa kanuni mpya ya Rais wa Baraza Kuu

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Mogens Lykketoft ametangaza leo kanuni mpya katika uongozi wa ofisi yake, huku nchi wanachama wakijadili leo marekebisho yanayohitjika ili Baraza Kuu liwe kweli bunge la mataifa. Taarifa zaidi na Priscilla Lecomte.

(Taarifa ya Priscilla)

Akizungumza leo kwenye ufunguzi wa mjadala huo, Bwana Lykketoft amesema marekebisho ya Baraza Kuu ni lazima ili kupata ufanisi katika utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu.

Amesema kipaumbele ni kuimarisha utendaji kazi wa ofisi ya Rais wa Baraza Kuu, wakati ambapo uchunguzi juu ya tuhuma za rushwa unafanyika dhidi ya Rais wa 68 wa Baraza hilo John Ashe.

Bwana Lykketoft ametangaza kanuni tatu mpya ili kuimarisha kiwango cha maadili na utawala bora kwenye ofisi yake.

(Sauti ya Bwana Lykketoft)

 “Kwanza umakinifu na uadilifu, ili kuwakilisha Baraza hilo bila upendeleo, na kuhakikishia usawa wa kijinsia na kijiografia. Pili uwazi na uwajibikaji, kwa kutoa taarifa kuhusu safara rasmi na matumizi. Tatu, utalaam na ufanisi.”