Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Juhudi maradufu zahitajika kuundwa serikali ya kitaifa Libya: UNSMIL

Juhudi maradufu zahitajika kuundwa serikali ya kitaifa Libya: UNSMIL

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya UNSMIL umewataka wadau wakuu nchini humo kuongeza juhudi maradufu katika kufikia suluhu la mchakato wa majadiliano ya kisiasa ya nchi hiyo ili kuruhusu kuundwa kwa serikali ya mkataba wa kitaifa na kuanza kwa mpito wa kidemokrasia.

Taarifa ya UNSMIL inasema kuwa mara baada ya kukamilika kwa majadiliano ya kisiasa ujumbe huo ilikabidhi kwa wadau kwa ajili ya kuidhinishwa na kuongeza kuwa ujumbe umefanya mashauriano na pande husika.

Mashauriano hayo ni kuhusu masuala ya uundwaji wa baraza la Rais, hususani uwakilishi Mashariki mjini Beghazi ili kusaidia katika kuweka urari katika masuala ya kijografia, na kikanda.

UNSMIL imefafanua kwamba pande zote zilikuwa katika makubaliano kuhusu madai hayo na uhitaji kwa kupanua uundwaji wa baraza la Rais kutoka sita hadi tisa ikiwamo Waziri Mkuu , Manaibu Mawaziri watano na Mawaziri watatu.