Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Miundo bora ya miji inaweza kupunguza madhara ya majanga na mabadiliko ya tabianchi- Ban

Miundo bora ya miji inaweza kupunguza madhara ya majanga na mabadiliko ya tabianchi- Ban

Ikiwa leo ni Siku ya Miji Duniani, Katiobu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amesema kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu – ‘imeundwa kwa kuishi pamoja’ – inaonyesha mchango muhimu wa miundo ya miji katika kujenga mazingira ya miji endelevu, fanisi na yanayostahili kijamii.

Katibu Mkuu amesema miundo mizuri ya miji inaweza kusaidia kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kupunguza madhara ya majanga.

Aidha, Ban amesema miundo mizuri ya miji inaweza kuifanya iwe salama zaidi, safi zaidi na yenye usawa zaidi. Ameongeza kuwa miundo mizuri ya miji pia huendeleza usawa katika upatikanaji wa huduma, ajira na fursa, na kuwafanya watu waridhike.