Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yaanza kampeni ya chanjo dhidi ya Kipindupindu Iraq

WHO yaanza kampeni ya chanjo dhidi ya Kipindupindu Iraq

Shirika la Afya Duniani, WHO limesema litaanza kampeni kubwa ya chanjo dhidi ya Kipindupindu wiki hii, nchini Iraq, huku likionya umuhimu wa kuwa katika hali ya juu ya tahadhari ya kuzuka kwa ugonjwa nchini Syria.

Kufikia sasa, WHO imesajili visa karibu 2000 vya maambukizi nchini Iraq, ambapo watu wawili wamefariki dunia baada ya kuambukizwa kipindupindu.

Huku hayo yakijiri, nchini Syria onyo limetolewa baada ya kijana mwenye umri wa miaka mitano katika mkoa wa Aleppo kufariki dunia , japo haijadhibitishwa kama kifo chake kilisababishwa na Kipindupindu.

Christian Lindmeier ni msemaji wa WHO hapa anaelezea utaratibu huo wa chanjo nchini Iraq

“Bila shaka, haitoshi kumchanja kila mtu, lakini hii itakuwa chanjo ya kimkakati ya kuzuia njia ya maambukizi zaidi ya bakteria anayesababisha kipindupindu”