Skip to main content

Bustani za kaya zaleta nuru Lesotho licha ya mabadiliko ya tabianchi:FAO

Bustani za kaya zaleta nuru Lesotho licha ya mabadiliko ya tabianchi:FAO

Wakati mabadiliko ya tabianchi yanazidi kuleta machungu maeneo mbalimbali duniani ikiwemo Lesotho, Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO linashirikiana na serikali ya nchi hiyo na wadau wake kutekeleza mkakati wa kukabiliana na mabadiliko hayo ili kuimarisha kilimo.

Mratibu wa masuala ya dharura wa FAO nchini Lesotho Borja Miguelez amesema mkakati huo unaboresha mfumo wa kilimo kustahimili mabadiliko ya mwelekeo wa mvua na viwango vya juu vya joto ambapo unalenga kuendeleza kilimo cha bustani kwenye kaya na kiwe cha kisasa zaidi.

Mfumo huo wa bustani unahusisha tuta lililoinuliwa juu na kushikiliwa na mawe linawekewa tundu lenye kipenyo cha mita mbili na linakuwa na udongo wenye rutuba, majivu na mbolea ya samadi na hivyo kuwezesha kilimo cha pamoja cha karoti na spinachi.

Makompi Mahlomola, kutoka kijiji cha Komeng nchini Lesotho ni mnufaika wa mpango huo.

(Sauti ya Makompi)

“Bustani yetu ya nyumbani imetusaidia sana kwa sababu tunaweza kulima mboga kwa kipindi kirefu hata wakati wa kipindi cha ukame. Spinachi ni nzuri sana kwani inaweza kulimwa katika kipindi chote cha mwaka.”