Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ulaya, zuieni usafirishaji haramu wa binadamu: Mtaalamu huru

Ulaya, zuieni usafirishaji haramu wa binadamu: Mtaalamu huru

Nchi za Ulaya zimetakiwa kuzuia usafirishaji haramu wa binadamu na kulinda haki za watu walio katika hatari.

Idadi kubwa ya watu wanakimbilia Ulaya kutoka Mashariki ya Kati na Afika wakiepuka  machafuko na adha, na wengi wao huishia katika mikono ya wasafirishaji haramu wa binadamu na hivyo kusafirishwa kinyume cha sheria.

Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa zaidi ya watu 3,000 wamekufa katika bahari ya Mediterenia wakati wakijaribu kufika Ulaya mwaka 2015.

Ikiwa leo ni siku kupinga usafirishaji wa binadamu barani Ulaya, Mtaalamu huru wa Umoja wa Maataifa kuhusu suala hilo Maria Grazia Giammarinaro ametaka bara hilo kuongeza bidii katika kutoa ulinzi dhidi ya watu walioko hatarini kusafirishwa.

Ametaka Umoja wa Ulaya, EU kuhakikisha sera za kupinga usafirishaji wa binadamu haziathiriwi na kile alichokiita sera marufuku za wahamiaji na zisizo jumuishi. Amesema sera hizo zinaweza kuongeza hatari kwa uhamiaji na unyanyasaji kwa watu.