Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kampeni kuzinduliwa kutokomeza aina mpya za utumwa duniani

Kampeni kuzinduliwa kutokomeza aina mpya za utumwa duniani

Shirika la kazi duniani, ILO kwa kushirikiana na wadau wake kesho litazindua kampeni kubwa mpya yenye lengo la kutokomeza aina mpya ya utumwa ulimwenguni.Taarifa kamili na Grace Kaneiya.

(Taarifa ya Grace)

Kampeni hiyo inalenga kusaka uungwaji mkono wa umma na kushawishi angalau nchi 50 ziwe zimeridhia itifaki ya shirika hilo ya kupinga utumikishwaji ifikapo mwaka 2018.

Itifaki hiyo iliyopitishwa na nchi wanachama wa ILO mwaka 2014 ina nguvu kisheria na inajumuisha mikakati ya kuzuia, kulinda na kufidia aina zote za utumikishaji zinazohusishwa na aina mpya za utumwa duniani.

Miongoni mwa wadau wa mpango huo ni shirikisho la waajiri duniani, IOE na shirikisho la vyama vya wafanyakazi duniani, ITUC.