Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Miaka 70 ya UM kilele chake mwishoni mwa wiki hii

Miaka 70 ya UM kilele chake mwishoni mwa wiki hii

Umoja wa Mataifa umeandaa tumbuizo maalum la kuadhimisha miaka 70 tangu kuanzishwa kwake.

Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Mkuu wa masuala ya mawasiliano ya Umma ndani ya Umoja huo, Cristina Gallach amewaambia waandishi wa habari jijini New York, Marekani kuwa kilele hicho kitashuhudia tumbuizo mbali mbali ikiwemo..

(Sauti ya Gallach)

“Tumbuizo kuu litatoka bendi ya Okestra ya shirika la utangazaji la Korea Kusini na wataungana na mjumbe wa amani wa Umoja wa Mataifa Lang Lang, pamoja na kwaya ya Harlem na waimbaji wa mtindo wa Pop kutoka Korea Kusini, Davichi.”

Bi. Gallach amesema kukamilika kwa tumbuizo hilo kutafuatiwa na majengo mbali mbali duniani kuangazia mwanga wa buluu ikiwa ni hatua ya kuonyesha mshikamano na chombo hicho kinachochagiza amani, usalama, maendeleo na haki za binadamu duniani.

Kuangaza buluu kutaanzia Australia, halafu Asia ikifuatia na Afrika na kumalizikia Amerika.