Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR, Marekani wachangia wakimbizi

UNHCR, Marekani wachangia wakimbizi

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR kwa kushirikiana na serikali ya Marekani wanachangisha fedha kwa ajili ya kusaidia wakimbizi ambapo kiasi cha dola milioni moja tayari kimechangwa.

Katika mahojiano na redio ya Umoja wa Mataifa Janeffer Patterson  amesema kampeni hiyo maalum ya uchangaji wa fedha ni kuitikia kile Marekani ilichosema wakati wa mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa hivi karibuni  ambapo ilitaka sekta binafasi kushirikiana katika kusaidia zaidi wakimbizi.

Bi Janeffer amesema kampeni hii pia inahusisha elimu kwa uma kwa raia wa Marekani kuhusu wakimbizi

(SAUTI JANEFFER)

‘‘Tunafurasia sana kuhusu uwezekano wa kutoa elimu kwa uma wa Marekani kuhusu wakimbizi ambalo halijulikani vyema. Hapa Marekani hatuna wakimbizi kwahiyo elimu ni muhimu kadri fedha zitakavyokuwa zinachangwa.