Skip to main content

Mafuriko ni Tishio la Kimataifa, UM

Mafuriko ni Tishio la Kimataifa, UM

Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kupunguza hatari ya majanga, UNISDR, Margareta Wahlström leo amesema maeneo ya mijini ni lazima yawekeza zaidi katika kupunguza hatari zitokanazo na mafuriko. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi.

(Taarifa ya Assumpta)

Katika taarifa yake, Bi. Walhstrom ametolea mfano mafuriko na maporomoko ya udongo yalivyosababisha vifo vya mamia ya watu nchini Guatemala, na jimbo la South Carolina nchini Marekani pamoja na maeneo ya Kusini mwa Ufaransa hivi karibuni.

Amesema mafuriko yanayoandamana  na maporomoko ya udongo na mvua kali isiyo ya kawaida wakati mwingine, yamekuwa hali ya kawaida ya tabianchi katika maeneo yote katika kipindi cha miaka 20 iliyopita.

Katika Muktadha hiyo, Mkuu huyo wa UNISDR ameongeza kuwa, sayansi inatueleza ni lazima tutarajie mvua kubwa zaidi katika maeneo mengi ya dunia, kwa sababu ya mabadiliko ya tabianchi, na ukweli ni kwamba, hewa ya ukaa  ni asilimia 43% zaidi ya viwango vya kabla ya kipindi cha upanuzi wa viwanda Ulaya.