Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto 500 hufariki dunia kila siku wakienda shuleni:WHO

Watoto 500 hufariki dunia kila siku wakienda shuleni:WHO

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kutembea kwa mguu kwenda shuleni, ripoti zinaonyesha kuwa watoto 500 hufariki dunia kila siku kwenye ajali za barabarani pindi wanapokwenda shuleni. Taarifa zaidi na Amina Hassan.

(Taarifa yaAmina)

Takwimu hizo ni kwa mujibu wa shirika la afya duniani, WHO ambapo imesema watoto hao hupata ajali hizo barabarani wanapokuwa wanakwenda kusaka elimu shuleni.

Nats..(filamu sauti)

Ili kuongeza ufahamu wa jamii kuhusu tatizo hilo, mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu usalama barabarani, Jean Todt kwa kushirikiana na shirikisho la kimataifa la magari, FIA wameshirikiana na mtengeneza filamu Luc Besson kuandaa filamu kuimarisha usalama wa watoto barabarani duniani kote.

Filamu hii iliyotengenzwa Afrika Kusini na Ufaransa inaonyesha hatari wanazopata watoto barabarani tangu wanapoamka asubuhi kwenda shuleni.

Hatari hizo zinatokana na pengine ukosefu wa miundombinu bora ya kuwawezesha kwenda shuleni salama au msongamano wa magari unavyoweza kuwa  hatari kwa watoto