Marekebisho yahitajika rasimu kuhusu mabadiliko ya tabianchi: Muyungi

Marekebisho yahitajika rasimu kuhusu mabadiliko ya tabianchi: Muyungi

Siku moja baada ya rasimu ya kwanza ya kina kuhusu mkataba mpya kuhusu tabianchi duniani kutolewa, mmoja wa wawakilishi wakuu wa Afrika kwenye mashauriano ya mkataba huo amesema kimsingi nyaraka hiyo ina mwelekeo sahihi lakini bado kuna masuala ya kuangalia ili iweze kukidhi mahitaji.

Richard Muyungi akizungumza na idhaa hii kwa njia ya simu amesema wote wanakubali kimsingi kuwa hatua za haraka zinapaswa kuchukuliwa kukabili mabadiliko ya tabianchi lakini rasimu hiyo..

(Sauti ya Muyungi)

Akagusia pia uwajibishaji wa nchi ambazo hazitatekeleza wajibu wake akisema kunahitajika marekebisho.

(Sauti ya Muyungi)

Kwa mujibu wa Muyungi, tarehe 20 mwezi huu mashauriano yatafanyika zaidi huko Bonn, Ujerumani akisema ni fursa ya kuboresha nyaraka hiyo.