Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akutana na Waziri Javad Zarif wa Iran

Ban akutana na Waziri Javad Zarif wa Iran

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, leo amekutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Javad Zarif.

Kuhusu suala la nyuklia nchini Iran, Katibu Mkuu ametoa wito kwa pande husika kutekeleza makubaliano ya nyuklia, yaani mpango wa pamoja wa kina wa kuchukua hatua, kwa moyo mwema.

Halikadhalika, Katibu Mkuu na Waziri Zarif wamejadili kuhusu masuala ya kikanda, yakiwemo Syria, Yemen na Lebanon.

Kuhusu Syria, Katibu Mkuu amekariri kuwa hakuna suluhu la kijeshi kwa mzozo ulioko nchini humo, na kuiomba Iran itumie ushawishi wake kuchagiza suluhu la kisiasa.

Kuhusu Yemen, Ban amefanyia tathmini juhudi za mjumbe wake maalum kuanzisha tena mazungumzo kwa misingi ya maazimio husika ya Baraza la Usalama.

Na kuhusu Lebanon, Katibu Mkuu amesisitiza haja ya kujaza pengo la urais nchini humo haraka iwezekanavyo.