Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

SDGS ni muhimu kwa ustawi wa nchi ninazoendelea: Ban

SDGS ni muhimu kwa ustawi wa nchi ninazoendelea: Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon amesema ajenda ya maendeleo endelevu SGDS inayozinduliwa  ijumaa hii jijini New York sio tu kwamba ni jumuishi lakini pia itatoa fursa kwa nchi zinazoendelea kupiga hatua  kupitia mipango ya ndani na sera.

Akihutubia mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa kundi la nchi 77 na China, Ban amesema SDGS itasaidia nchi zinazoendlea kupitia ushirikiano wa maendeleo kwani agenda hiyo itainua ubia  wa kimataifa kwa ajili ya maendeleo.

(SAUTI BAN)

‘Ni ajenda ambayo imejikita  kwa watu na ni rafiki kwa sayari. Ni ajenda inayojenga  dunia yenye amani ambayo inaongozwa na kanuni za haki na mshikamano na kujali kizazi kijacho na sayari dunia.’’

Katibu Mkuu amesema agenda 2030 kadhalika ni muhimu kwani inashughulikia ulinzi wa sayari dunia na kukabailiana na mabadiliko ya tabia nchi.