Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ajenda 2030 na nuru kwa maisha ya watoto na vijana: Eliasson

Ajenda 2030 na nuru kwa maisha ya watoto na vijana: Eliasson

Siku moja kabla ya kuanza kwa mkutano wa kupitisha malengo ya maendeleo endelevu, Umoja wa Mataifa umekuwa na mkutano wa kuangazia malengo hayo na fursa zake kwa mtoto ambapo Naibu Katibu Mkuu Jan Eliasson amesema ajenda mpya inatoa nurukwa watoto. Assumpta Massoi na taarifa zaidi.

(Taarifa ya Assumpta)

Watoto na malengo ya maendeleo endelevu, kumpatia fursa kila mtoto, ndiyo mada ya mkutano huo ukizingatia kuwa kila mtoto ana haki ya kuishi bila woga na kwamba kuchanua ndiyo msingi na wajibu wa kimaadili ya kibinadamu.

Akihutubia washiriki, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson amesema ukosefu wa lishe bora, elimu sambamba na kukumbwa na mateso ni miongoni mwa madhila mengi yanayokumba watoto duniani bila kusahau wale walio katika mazingira magumu, hivyo mategemeo ni ajenda 2030 kwani

(Sauti ya Eliasson)

“Lengo namba 16 linajumuisha lengo dogo, na nanukuu..”Kutokomeza manyanyaso, utumikishaji, usafirishaji haramu wa watoto na aina zote za ukatili na mateso dhidi ya watoto, likiunganishwa na mkataba wa kimataifa wa haki za mtoto. Kila siku tunaona jinsi watoto wakimbizi walivyo hatarini kukumwba na madhila.”

Pamoja na watoto amesema matarajio pia kwa ajenda hiyo ni kuinua fursa za ajira zeye utu kwa vijana ili nao waweze kuchangia katika ustawi endelevu wa dunia.