Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Benki ya dunia yakomboa wavuvi na wakulima wa mwani Zanzibar

Benki ya dunia yakomboa wavuvi na wakulima wa mwani Zanzibar

Malengo ya maendeleo endelevu, SDGs yanaridhiwa baadaye mwezi huu katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa na viongozi 193 wa nchi wanachama wa Umoja huo. Malengo hayo yako 17 na miongoni mwao ni lile namba moja linalohusika zaidi na kumaliza umaskini uliokithiri ifikapo mwaka 2030. Huko Zanzibar nchini Tanzania, tayari Benki ya dunia imeona changamoto ambazo zinaweza kuwa kikwazo cha kufikia lengo hilo ambalo lilianzia wakati wa utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya milenia, MDG. Je ni kitu gani benki hiyo inafanya? Na ni kwa sababu gani? Basi  ungana na Assumpta Massoi anayetupeleka kisiwani huko kupitia makala hii.