Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuna maendeleo, lakini bado kuna kazi kuhusu Mpango wa Nyuklia Wa Iran, IAEA

Kuna maendeleo, lakini bado kuna kazi kuhusu Mpango wa Nyuklia Wa Iran, IAEA

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la nishati ya atomiki la Umoja wa Mataifa, IAEA, Yukiya Amano ameelezea bodi ya shirika hilo kuhusu ziara yake ya mwishoni mwa wiki nchini Iran, ambapo alifanya mazungumzo na Rais wa nchi hiyo Hassan Rouhani na wakuu wengine wa serikali sambamba na wabunge. Kwa maelezo zaidi, huyu hapa Grace Kaneiya.

(Taarifa ya Grace)

Katika maelezo yake kwa bodi, Amano amesema maendeleo makubwa yamefikiwa katika utekelezaji wa mpango wa nyuklia ya amani ya Iran.

Aidha, Amano amesema alitembelea eneo la Parchin, ambalo alisema mara nyingi ni muhimu katika kubaini uwezekano wa Iran kutumia mradi wake wa nyuklia kwa sababu ya kijeshi.

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa IAEA, Tero Varjoranta pia alikuwa kwenye ziara hiyo, hii ikiwa mara ya kwanza kwa shirika hilo kuwahi kutembelea eneo hilo.

Hata hivyo, Amano ameonya kuwa bado kuna kazi kubwa ya kufanywa katika kipindi cha wiki ijayo katika utekelezaji kikamilifu wa mpango wa nyuklia kwa matumizi ya amani nchini Iran.