Mizozo yazidi kusambaratisha dunia: Ban

Mizozo yazidi kusambaratisha dunia: Ban

Leo ni siku ya amani duniani ambapo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa Katibu Mkuu Ban Ki-moon ameongoza katika tukio hilo la kila mwaka akisema mizozo inazidi kuigawa dunia na hali ya binadamu inakuwa mashakani. Taarifa zaidi na Amina Hassan.

(Taarifa ya Amina)

Nats..

Tumbuizo katika bustani za Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani katika maadhimisho ya siku ya amani, tumbuizo lililofuatiwa na hotuba ya Katibu Mkuu Ban akisema amani inakabiliwa na changamoto hata katika nchi zenye demokrasia thabiti..

(Sauti ya Ban)

“Watu wanaumia kwa sababu ya chuki na ghasia, wanawake wanashambuliwa kwa sababu ya jinsi yao. Umaskini nao ni janga lingine, watoto wanakufa kwa utapiamlo katika dunia hii yenye chakula kingi.”

Kisha akagonga kengele ya amani…..

Na ndipo Rais wa Baraza Kuu Morgens Lykketoft akafunguka..

(Sauti ya Mogens)

"Hebu na kengele hii ya amani ilie kwa ajili ya kuwasifu viongozi ambao wamechagua njia ya mashauriano na amani badala ya uvamizi wa amani.”