Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IAEA na mkakati wa kuongeza wanawake katika sayansi ya nyukilia

IAEA na mkakati wa kuongeza wanawake katika sayansi ya nyukilia

Licha ya kuongezeka kwa idadi ya wanawake katika fani ya nyuklia  Shirika la Umoja wa Mataifa la Nishati ya Atomiki IAEA, linasema idadi hiyo ni ndogo ikilinganishwa na wanaume, hasa kwa kulinganisha pengo kati ya wahitimu wa vyuo vikuu katika fani hiyo.

Katika mahojiano na redio ya Umoja wa Mataifa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa IAEA Janice Dunn-Lee anasema ni muhimu kuwahamasisha wanafunzi wa kike kujiunga katika masomo ya sayansi ili kuwa na wanawake wengi zaidi katika fani ya nyukilia.

(SAUTI JANICE)

‘‘Tunapigia chepuo IAEA kwamba ni chaguo tazamiwa la ajira na kuwahamasisha wanafunzi kuchukua masomo ya fani ya nyuklia kwani ni fani ambayo haijumuishi sayansi na tekenolojia pekee bali pia sheria, diplomasia na usimamizi.’’

Katika ufunguzi wa mkutano mkuu wa 59 wa IAEA Mkurugnezi Mkuu wa shirika hilo alieleza mchango mkubwa wa wanawake katika masuala ya nyukilia yanayoratibiwa na IAEA.