Nyuklia yatumiwa kuimarisha uzalishaji wa kilimo nchini Kenya

Nyuklia yatumiwa kuimarisha uzalishaji wa kilimo nchini Kenya

Teknolojia za nyuklia zinaweza kuchangia katika kukuza sekta ya kilimo rafiki kwa mazingira, kwa kuzuia momonyoko wa ardhi, kuimarisha uzalishaji na matumizi ya maji.

Hii ni kwa mujibu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Umoja wa Mataifa IAEA, linalokutana mjini Vienna, Austria  wiki hii kwa ajili ya kongamano lake la kila mwaka.

Mwaka huu ukiwa ni mwaka wa kimataifa wa ardhi, IAEA imesisitiza kwamba kutunza udongo ni msingi wa kupambana na mabadiliko ya tabianchi.

Isaya Sijali, mwanasayansi kutoka shirika la utafiti kuhusu kilimo na mifugo ya Kenya, KALRO, ni mmoja wa washiriki wa kongamano hilo na anaelezea zaidi.

(Sauti ya Isaya)