Skip to main content

Sheria ifuate mkondo kudhibiti unyanyasaji wa kingono mizozoni: Ban

Sheria ifuate mkondo kudhibiti unyanyasaji wa kingono mizozoni: Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema ni lazima kuwa thabiti katika kuchukua hatua stahiki dhidi ya tuhuma za unyanyasaji wa kingono zinazofanywa na walinzi wa amani au wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa katika maeneo mbalimbali.

Akizungumza katika mkutano wa nchi zinazochangia vikosi vya ulinzi wa amani vya umoja huo, Ban amesema ni lazima uchunguzi wa kina ufanyike na akaongeza..

(SAUTI BAN)

"Lazima tuhakikishe haki inatendeka, nahuzunishwa kwamba kesi chache zimefikishwa mahakamani na adhabu hazitekelezwi ipasavyo.  Nazitaka nchi wanachama kuchukua hatua madhubuti kuhakikisha kwamba wanaothibitika kuhusika katika unyanyasaji wa kingono wanafikishwa katika vyombo vya sheria.’’

Bwana Ban amesema ni aibu na inatia hasira kufuatia tuhuma za unyanyasaji wa kingono dhidi ya watoto huko Jamhuri ya Afrika  ya Kati ambapo walinda amani kutoka Ufaransa wametuhumiwa kuhusika.