Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kesi dhidi ya Ntaganda kuanza kesho The Hague

Kesi dhidi ya Ntaganda kuanza kesho The Hague

Kesi dhidi ya Bosco Ntaganda itaanza kesho Jumatano kwenye makao makuu ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC huko The Hague, Uholanzi.

ICC imesema Jaji Robert Fremr ataongoza jopo la kusikiliza kesi hiyo akishirikiana na Jaji Kuniko Ozaki na Jaji Chang-ho Chung.

Ntaganda anakabiliwa na mashtaka 13 ya uhalifu wa kivita na matano ya uhalifu wa kibinadamu anayodaiwa kutenda huko Ituri, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kati yam waka 2002-2003.

Taarifa za utangulizi zitasomwa na mwendesha mashtaka wa ICC, upande wa utetezi na wawakilishi wa wahanga wa vitendo vya uhalifu wa binadamu vinavyodaiwa kufanywa na Ntaganda.

Halikadhalika upande wa mashtaka unatarajiwa kuanza kuwasilisha shuhuda za shahidi wa kwanza tarehe 15 mwezi huu.