Msaada zaidi watakiwa katika maeneo yaliyofunguliwa Somalia

21 Agosti 2015

Baada ya ziara za kufanya tathmini katika maeneo ya Gedo na Bay nchini Somalia, Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu nchini humo, Peter de Clercq amesema, msaada zaidi unahitajika kwa watu waliokuwa wakiishi katika maeneo yasiofikika kutokana na kuzorota kwa usalama nchini humo. Taarifa kamili na John Kibego.

(Taarifa ya Kibego)

Bwana de Clercq aliyetembelea miji ya Baardheere and Diinsoor amesema, licha ya watu kuanza kufikiwa na msaada, baado kuna uhitaji wa misaada ya dharura huhusani kwa wanaorudi makwao katika maeneo yalioathiriwa na harakati za kijeshi za hivi karibuni, ambapo hospitali ziliporwa na kuchomwa moto.

Amesema, ingawa shule zinatarajiwa kufungua hivi karibuni, hakuna walimu na miundonbinu katika miji hiyo miwili ambako chakula, maji safi na huduma zingine za msingi baado ni haba.

Bwana de Clercq ameongeza kuwa msaada zaidi pia unahitajika katika kilimo na ufugaji, kwani watu wameishi kwa karibu muongo mmoja bila mbegu bora wala kupata chanjo ya mifugo, ambavyo ni muhimu kwa chakula na mapato yao.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter