Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM walaani mashambulizi ya ndege Syria

UM walaani mashambulizi ya ndege Syria

Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Syria Staffan de Mistura, amelaani mashambulio ya ndege kwenye mji wa Duma nchini humo ambako watu kadhaa waliuwawa na wengine  kujeruhiwa. Taarifa kamili na John Kibego.

(Taarifa ya John Kibego)

Bwana de Mistura amesema, shambulio la jana dhidi ya watu waliokuwa sokoni ni dalili ya ukatili katika mzozo unaoendelea nchini Syria na kuzitaka pande zinazozozana kusitisha mapigano na kurejea kwenye meza ya mazungmuzo, kwani mzozo huo umeonekana kutopata suluhu la kijeshi kwa miaka kadhaa.

Amesisitiza kuwa, serikali kushambulia kiholela maeneo ya raia kwa mabomu na kuua takriban watu milioni moja ni marufuku kulingana na sheria za kimataifa.

Shambulio hilo limetokea muda mfupi baada ya uvurumishwaji wa makombora dhidi ya mji mkuu Damascas na vukundi vilivyojihami ambavyo vinapinga serikali ya Syria wiki iliyopita, uliyoathiri zaidi raia baada ya mifumo ya maji pia kukatwa .

Bwana de Mistura ametaka pande kinzani kuruhusu misaada ya kibinadamu iwafikie waathirika bila masharti yoyote na kutaka mauaji kukomeshwa hima.