Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama lahitimisha ziara Afghnanistan

Wajumbe wa baraza la Usalama la Umoja wa mataifa ziarani nchini Afghanistan. Picha: UM

Baraza la usalama lahitimisha ziara Afghnanistan

Wajumbe wa baraza la Usalama la Umoja wa mataifa leo wamehitimisha ziara nchini Afghanistan iliyoanza tarehe 13 mwezi huu , ikiwa ni ziara yao ya kwanza baada ya miaka saba. Selina Jerobon na tarifa kamili

(TAARIFA YA SELINA JEROBON)

Ziara ya mwisho ya wajumbe wa baraza la usalama nchini humo ilikuwa mwaka 2010, na ziara hii imekuwa ni fursa nzuri ya wajumbe hao  kukariri uungaji mkono wa baraza la Usalama kwa serikali na watu wa Afghanistan katika juhudi zao za kurejesha amani,  uthabiti na maendekleo kwa taifa.

image
Nikki Haley(kuli) na Mtendaji Mkuu wa Afghanistan Abdullah Abdullah pamoja na wajumbe wengine katika jumba ya Rais,  Sepedar huko Kabul, Afghanistan. Picha: UM
Lengo la safari ya wajumbe wa baraza hilo lilikuwa kujionea wenyeye maendeleo yaliyofanywa na serikali ya Umoja wa kitaifa wa Afghanistan, kwa msaada wa jamii ya kimataifa, katika kushughulikia  changamoto kadhaa na pia  kuona jinsi baraza la usalama linavyoweza kusaidia zaidi juhudi  hizo.

Kiongozi wa msafara huo, balozi, Kairat Umarov, ambae ni mjumbe wa kudumu katika Umoja wa Mataifa, aliandamana na  wajumbe kutoka Marekani, Uingereza, Ufaransa pamoja na wengine kutoka mataifa 14.

(SAUTI YA BALOZI UMAROV CUT)

image
Rais Ashraf Ghani na bibiye Mwanamke wa Kwanza Bi. Rula Ghani katika mkutano na wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa huko Kabul, Afghanistan
Ujumbe wa baraza hilo ukiwa mjini Kabul, ulikutana kwa mazungumzo na vigogo kadhaa  wa serikali akiwemo rais Ashraf Ghani na pia kukutana na wabunge wa bunge la taifa, asasi za akina mama na wajumbe wa mashirika mengi mengineyo.

Mazungumzo yao yalijikita katika  masuala ya siasa, uchumi na haki za binadamu yalivyo kwa sasa  nchini humo.

Ziara hii imekuja kabla ya mkutano wa Kabul uliopangwa  kufanyika Febuari 2018 ambapo serikali inatarajiwa  kutoa mwongozo wa mipango yake kuhusu michakato ya amani  pamoja na usalama